Belarus Yathibitisha Kifo cha Kwanza cha Mwandamanaji


Belarus imethibitisha kifo cha kijana mmoja hapo jana aliyekuwa anashikiliwa kizuizini kufuatia maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo. Kijana huyo alifariki dunia baada ya kuhamishwa gereza.
 Kamati ya uchunguzi imesema kwenye taarifa yake kwamba kijana huyo wa miaka 25 alifariki baada ya kukamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Gomel, kusinimashariki mwa nchi hiyo na kufungwa kwa siku kumi gerezani.

Wachunguzi hao wamesema chanzo cha kifo bado hakijajulikana. Kituo cha radio cha Free Europe/Radio Liberty kilimnukuu mama wa kijana huyo akisema mwanae alikuwa na matatizo ya moyo na alishikiliwa kwa muda mrefu kwenye gari ya polisi.

Kifo hiki cha karibuni kinaripotiwa wakati waandamanaji wa upinzani wakiandamana kupinga ukatili wa polisi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments