8/14/2020

Ben Pol, Mrembo Bilionea Kimenuka!


Mamb o sio mambo! Staa wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’ na yule mkewe bilionea wa Kenya, Anerlisa Muigai wamedaiwa kuwa kwenye ugomvi uliosababisha wamwagane.


Taarifa ambayo imeandikwa kwenye mitandao tofauti ya nchini Kenya, imeeleza kuwa mrembo huyo hayupo sawa na Ben Pol, na kwamba kuonesha hana mpango tena na staa huyo, amefuta picha zote za harusi ya kimila ambazo alikuwa ameziposti kwenye ukurasa wake wa Instagram.

“Anerlisa alikuwa ameposti picha nyingi tu za ndoa, na kama unakumbuka alisema atakamilisha tu kwa ndoa ya kanisani, lakini hata hivyo inaonekana ndoa hiyo imeyeyuka,” alieleza mtoa taarifa kwenye mtandao huo.

Mitandao hiyo inayoaminika kwa habari za mastaa nchini Kenya imeandika, mbali na watu wa karibu na mrembo huyo kuvujisha kwamba wawili hao wameachana, mrembo huyo pia amevua pete ya harusi ambayo alivalishwa na Ben Pol.

“Hana pete sasa hivi, ameshaivua kabisa. Sasa hivi bi dada anajiachia akiwa hana pete kabisa kidoleni,” kilieleza chanzo.
Hata hivyo, mitandao hiyo iliyoripoti habari hiyo, ilishindwa kumpata Anerlisa mwenyewe ili aweze kueleza kwa undani kwa nini amefikia hatua hiyo.


Risasi Mchanganyiko liliingia kwenye ukurasa wa Instagram na mrembo huyo na kujiridhisha kweli amefuta picha zake za harusi ambazo zilikuwa zinamuonesha akiwa na Ben Pol siku alipomvalisha pete na kuacha picha nyingine alizokuwa peke yake.


Kama hiyo haitoshi, Risasi Mchanganyiko lilijiridhisha kwamba picha za karibuni alizoposti mrembo huyo, zilimuonesha akiwa hana pete ya ndoa, japo zipo pia za nyuma zinazomuonesha akiwa na pete hiyo.

Risasi Mchanganyiko lilijaribu kumvutia waya Ben Pol ili kumsikia anazungumziaje suala hilo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Jitihada zaidi za kumtafuta zinaendelea!


Penzi la Anerlisa na Ben Pol lilikuwa gumzo miaka kadhaa iliyopita ambapo kapo yao ilipendwa sana mitandaoni. Mrembo huyo kutoka Kenya, ni bilionea aliyewekeza kwenye miradi mbalimbali ikiwemo kiwanda cha maji ya kunywa.

Stori | Memorise Richard, Risasi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger