8/16/2020

BREAKING: Haji Manara Atangaza Kustaafu SIMBA “Nipo SIMBA”MSEMAJI wa Simba SC, Haji Manara, leo Agosti 16, 2020 akizungumza na waandishi wa habari  makao makuu ya Simba, Msimbazi jijini Dar es Salaam, amesema ataomba kupumzika kidogo kutokana na afya yake kutokuwa sawasawa.


“Afya yangu siyo sawasawa madhubuti labda mnaweza mkashangaa…Nisiwakwaze, mnaweza mkashangaa baada ya muda mchache ujao nikawaomba kupumzika na nitumie furusa hii kuwaambia nipo Simba nitawaomba Wanasimba nipumzike kidogo kwa sababu ya afya yangu siyo madhubuti sawasawa, nitaendelea kuhamasisha nje ya Simba. Asanteni sana,” -Amesema Haji Manara.


Haji ameyasema hayo baada ya baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba kushiriki dua maalum ya kuiombea klabu hiyo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger