Breaking NEWS: Moto Waua 10 Baada ya Watu Kunasa Kwenye Jengo la Wagonjwa wa Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Watu 10 wamekufa leo katika ajali ya moto uliozuka kwenye hoteli moja iliyogeuzwa kuwa kambi ya wagonjwa wa COVID-19 katika mji wa kusini ya India wa Vijayawada.

Jengo hilo, lililokodiwa na hospitali binafsi limekuwa likitumiwa kuwaweka wagonjwa wa COVID-19 wenye dalili ndogo na ambao hawakuhitaji kulazwa hospitali.

Kulingana na polisi ya mji huo, moto ulizuka mapema leo asubuhi na vyombo vya habari vya eneo hilo vilionesha watu wakiwa wamekwama ghorofani.

Watu wengine 20 waliokolewa na sasa wanatibiwa katika upande mwingine wa hospitali na polisi inashuku moto huo huenda ulisababishwa na hitilafu ya umeme.

India imeshuhudia wimbi kubwa la maambukzii ya virusi vya corona ambapo jana iliripoti visa vipya 64,399 vya COVID.19 na kufanya idadi jumla ya mamabukzii kufikia milioni 2.2.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad