8/10/2020

Bwana Harusi Azirai Mbele ya Umma, Bi Harusi Afichua Ana Watoto WanneBiblia husema kuwa apataye mke hupata kitu chema. Methali hii iliingia vumbi katika eneo la Borabu, kaunti ya Kisii baada ya sherehe moja ya harusi iliyopangwa kwa hali ya juu kufikia kikomo ghafla kileleni.

Katika kisa hicho kilichofanyika Jumapili, Agosti 9, wenyeji pamoja na wageni waliohudhuria sherehe ya kukata na shoka Wiberforce Omwenga akifunga pingu za maisha na kipenzi cha roho walisalia vinywa wazi baada ya bwana harusi kuzirai ghafla.

Kulingana na mdaku wetu, kila kitu kilisambaratika pale mchungaji alipokuwa tayari kuwaunganisa rasmi wawili hao ambao walikuwa wapenzi wa muda mrefu.

Kabla kutiana pete, mchungaji aliwaomba wawili hao kutoboleana siri ili kufunganishwa wakiwa huru.

Pale ndipo bibi harusi akainua mkono kusema jambo.
 .

Kabla kutiana pete, mchungaji aliwaomba wawili hao kutoboleana siri ili kufunganishwa wakiwa huru. Picha: Hisani

Wageni na wenyeji walitega masikio kwa makini kusikia ujumbe aliokuwa nao bibi harusi kwa mumewe.

Binti huyo alieleza kuwa alikuwa na watoto wanne ambao hadi wakati wa kufanya harusi hiyo hakuwa amemwambia mpenzi wake kuwahusu.

Bibi harusi alimwomba mumewe kumsamehe na kumkubali pamoja na wanawe hao.

La kushangaza ni kuwa bwana harusi alipoteza nguvu na kuzirai pale paple baada ya kusikia kuwa mrembo wake wa muda alikuwa na watoto na hukuwa amempasha habari.

Sherehe hiyo ilisimama huku mchunguja pamoja na wengine wakishirikiana katika kumpulizi ewa bwana huyi na kisha kumkimbiza hospitalini.

Haikubainika kilichofuata hata baada ya wageni na wenyeji kutawanyika kutoka katika sherehe hiyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger