8/30/2020

Carlinhos Kumbe Amekataa Ofa UrenoIMEELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga raia wa Angola, Carlos St’enio Fernandez ‘Carlinhos’ amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno na kuja kukipiga Jangwani.

Yanga chini ya wadhamini wao Kampuni ya GSM, hivi karibuni ilifanikisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyekuwa anakipiga Interclube ya nchini Angola kwa ajili ya msimu ujao.

Carlinhos ni kati ya washambuliaji waliokuwepo kwenye mipango ya muda mrefu kusajiliwa na Yanga katika kukiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na msimu mpya wa 2020/2021

Kwa mujibu wa Hersi, ujio wa mshambuliaji huyo Yanga umewashtua watu wengi Angola, kwani walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ureno.

“Ujio wa Carlinhos hapa Yanga umewashtua wadau wengi wa soka nchini Angola, kwani wengi walitarajia kumuona akienda kucheza soka Ulaya na siyo Yanga.

“Hiyo ni kutokana na kiwango kikubwa ambacho anacho hivi sasa kwani ni kati ya wachezaji nyota wanaotazamwa Angola, amekataa ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ureno.

“Carlinhos baba yake ni Mreno na mama yake ni Muangola, hivyo ni rahisi kwake kwenda kucheza kucheza soka huko Ureno,” alisema Hersi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger