8/01/2020

Chad: Watu 10 wamepoteza maisha katika shambulizi lililoandaliwa na kundi la Boko HaramWatu 10 wamepoteza maisha katika shambulizi lililoandaliwa na kundi la kigaidi Boko Haram katika bonde la Ziwa Chad magharibi mwa Chad. 


Kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya kitaifa, afisa wa jeshi hilo, ambaye hakutaka kutoa jina lake, amesema kwamba shambulio la silaha lilitekelezwa katika kijiji kilicho katika bonde la Ziwa Chad. 


Afisa huyo amesema kuwa wanawake 2 na wanaume 8 wamepoteza maisha yao na watu wengi wamejeruhiwa katika shambulizi hilo. 


Baada ya kugunduliwa kuwa watu 7 wametekwa nyara katika shambulizi hilo, ofisa huyo amesema kwamba wanamgambo wa Boko Haram walivamia kijiji hicho na kupora chakula.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger