8/01/2020

CHADEMA Kukutana kwa Siku Tatu Kuchagua Mgombea Urais, Wabunge, MadiwaniCHADEMA kinaingia siku tatu ngumu za mchakato wa kupata mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. 


 Chadema kitaanza mikutano yake kesho Jumapili tarehe 2-4 Agosti, 2020 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Pia, Chadema kitatumia mikutano hiyo, kuwapata wagombea ubunge, wawakilishi na madiwani wa viti maalum na wabunge wa viti maalum.

     

Kesho Jumapili, itakuwa ni kikao cha Kamati Kuu ya Chadema, Agosti 3, zamu ya Baraza Kuu na mwisho Agosti 4 itakuwa ni mkutano mkuu.


Awali, mikutano hiyo ilipangwa kufanyika kati ya tarehe 27 hadi 29 Julai 2020, lakini ikasogezwa mbele kutokana na msiba wa Hayati Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

2 comments:

 1. Dkt MayRose oyeee..!!
  Nyalandu Safiii...!!!

  Faru Joni na Faru Rajabu Twitter Safii.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mie naona Vibeko wajipange saccozi iko Hoi Bin Taaban.

   Sina uhakika na kodi ya Ufipa.
   huko Kisutu na mpangilio mzima wa Ruzuku kuishia kwa wana Boda boda na bajaji. Mbungo anaendelea na uchambuzi kama Karanga.

   Mnya Kigoda upo..?? Poa? Sabaya kiboko yao. Safii.

   Wajumbe safii? Hongereni sana.

   Delete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger