8/29/2020

CHADEMA wazindua kampeni, Lissu azungumza haya


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leo Agosti 28, 2020, kimefanya uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais kwenye viwanja vya Mbagala Zakhiem, ambapo Mgombea wa Kiti hicho cha Urais Tundu Lissu amesema, wanaanza kampeni wakiwa hawana wagombea 52 kati ya wagombea 244 waliowaweka.


Katika uzinduzi huo Lissu amesema kuwa hawategemei kujitoa kwenye uchaguzi na kwamba kuanzia leo katika kila mkutano wa kampeni hoja yao kubwa itakuwa ni ya kurudishwa kwa wagombea waliondolewa bila kuwekewa masharti yoyote.

"Hatutajitoa kwenye uchaguzi, tutakachofanya kuanzia leo nchi nzima, katika kila mkutano wa kampeni hoja yetu ni wagombea wetu walioondolewa kinyume cha sheria warudishwe bila masharti yoyote na hata wa vyama vingine warudishwe", amesema Lissu.

Aidha amesema kuwa hoja zao siyo kwa wagombea wa CHADEMA tu, bali hata vyama vingine ambavyo wagombea wao wameenguliwa
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger