8/10/2020

CHADEMA yataja majina ya wagombea wake wa Ubunge


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Asia Msangi kuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga, John Mrema kugombea Jimbo la Segerea, Halima Mdee Jimbo Kawe, Ubungo ni Boniface Jacob, Bagamoyo Emmanuel Lukumay, Kibaha Edward Kinabo, Kibiti Kulwa Lubuva, Mafia Omary Hassan.


Majina yaliyotajwa hii leo Agosti 9, 2020, yamehusisha Majimbo 163 kutoka katika kanda 8, ambazo ni kanda ya Kati, Kanda ya Nyasa, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Serengeti, Kanda ya Viktoria, Kanda ya Kusini, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Pwani.

Majina mengine yaliyochaguliwa kuwania ni pamoja na John Heche, wa jimbo la Tarime Vijijini, Ester Matiko Jimbo la Tarime Mjini, Ester Bulaya jimbo la Bunda Mjini, Godbless Lema jimbo la Arusha Mjini, Rebecca Mgondo Arumeru Mashariki, Jimbo la Siha ni Elvis Mos, Moshi Vijijini Lucy Ndesamburo, Rombo ni Patrick Assenga.

Aidha chama hicho pia kimewateua Leonard Ngonyani kugombea jimbo la Namtumbo, Ndanda ni Cator Joseph Mmuni, Nyamagana ni John Pambalu, Upendo Peneza Jimbo la Geita Mjini, Mbeya ni Joseph Mbilinyi, Serengeti ni Catherine Ruge.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger