CHADEMA yawataja warithi wa Mnyika na Lijualikali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Chama cha CHADEMA kimetaja awamu ya tatu ya majina ya wabunge wake watakaogombea katika Uchaguzi Mkuu ujao, wakiwemo warithi wa Jimbo la Kibamba lililokuwa likiongozwa na John Mnyika pamoja na la Kilombero lililokuwa chini ya Peter Lijualikali aliyekihama chama hicho na kwenda CCM.



Majina hayo ya awamu ya tatu yamewekwa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa chama hicho hii leo Agosti 17, 2020, ambapo chama hicho kimemteua Sina Manzi kugombea Jimbo la Temeke na Jimbo la Ilala akiteuliwa Hashim Issa.

Kwa upande wa Jimbo lililokuwa likiongozwa na John Mnyika, atakayegombea kwa mwaka huu ni Ernest Mgawe, huku Jimbo la Kilombero akiteuliwa Modestus Chitemi, Jimbo la Igunga ni Ngassa Mboje, Jimbo la Chamwino ni Samson Muhembano na Jimbo la Mchinga chama hicho kimemteua Mohamed Kamtande.

Wengine walioteuliwa hii leo ni wa Jimbo la Liwale ambaye ni Hamad Kamtande, Jimbo la Hanang na Magoma Derick Magoma, Jimbo la Kilwa Kaskazini ni Geofrey Kipengele, Jimbo la Solwa ni Mwinula Kasonzo.

Kwa upande wa John Mnyika, yeye alisema kuwa ameamua kutogombea Ubunge kwa mwaka huu na badala yake atajikita katika kujenga chama na kutumikia vyema majukumu yake ya Ukatibu Mkuu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad