8/18/2020

Chuchu Hansy afuata wosia Khadija Kopa "Wanaume ndivyo walivyo"


Mkongwe wa muziki wa Taarab Khadija Kopa amefunguka kumpa wosia msanii wa filamu Chuchu Hansy kuhusu matatizo ya kimaisha na wanaume baada ya kuwa na taarifa kwamba hayupo sawa na mzazi mwenziye Vincent Kigosi "Ray".


Akieleza zaidi kuhusiana na hilo Khadija Kopa amesema anamshukuru Chuchu Hansy kwa kutambua uwepo wake hadi kumfuata na kumpatia wosia na ushauri wa matatizo ya maisha na wanaume.

"Ahsante mwanangu Chuchu Hans kwa kutambua uwepo wangu kutokana na matatizo yako ya kimaisha na kuja kwangu kufuata wosia wangu, Ahsante kwa kunielewa na ukayafanyie kazi, Wanaume ndivyo walivyo usimalize maadam kakuomba msamaha basi huyo ni muungwana Mungu awajaalie muendelee na maisha mazuri" ameandika Khadija Kopa kupita mtandao wa Instagram

Kwa upande wa Chuchu Hansy amejibu kwa kuandika "Asante sana mama yangu Khadija Kopa kwa ushauri wako, nimekuelewa na nitafata kila kitu ulichoniambia nakushukuru sana"

Wiki iliyopita Chuchu Hansy aliweka taarifa kama hayupo sawa na mpenzi wake ambaye ni mzazi mwenziye Vinceuku akidai kama amesalitiwa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger