Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Dalili Kuu 7 zinazoonyesha mtu Ambaye Atachelewa Sana Kufanikiwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo  lakini hana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie, kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana MUDA wa Kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine. Huongea sana Kuliko Kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo ....

NDOTO YAKO INAWEZEKANA, CHUKUA HATUA.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE