8/28/2020

Dude apata ajali, akimbizwa HospitaliniMsanii wa filamu Bongo Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amekimbizwa Hospitali ya Magomeni Jijini Dar es Salaam baada ya kupata ajali ya bodaboda kwa kugongwa na gari la kubebea wagonjwa Ambulance.


Katibu wa wasanii wa filamu Jafari Makatu ameeleza kuwa, Dude alikuwa anawahi gari la wasanii ambao wanasafari ya kwenda Dodoma, alivyofika Magomeni Usalama akapata ajali iliyomsababishia majeraha kichwani.


"Kwa sasa tupo Hospitali Magomeni, alikuwa kwenye bodaboda akagongwa na Ambulance yeye na dereva wake wote wapo hospitali, amepata majeraha kichwani kwa hiyo ametoka kupiga Xray tunasikilizia majibu kama itashindikana tutamuhamishia Hospitali ya Rufaa wasanii wenzake wote wapo hapa hospitali, mwanzo alikuwa hawezi hata kuongea ila sasa hivi anaendelea vizuri kidogo" ameeleza Katibu wa wasanii Jafari Makatu HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger