8/04/2020

Exclusive: Snura Amwambia Shilole, ‘Acha Utoto’ – Video


MWANAMUZIKI wa singeli nchini, Snura Mushi, amejibu tuhuma zilizotolewa na mwanamuziki mwenzake, Zuwena Mohammed maarufu kwa jina la Shilole au Shishi Baby, dhidi yake kuwa alifurahia kitendo cha yeye kupigwa na mumewe Uchebe.

Akifanya Exclusive interview na Global TV Online, Snura amesema; “Mimi siwezi kufurahia matatizo ya mwenzangu, kwani ni kama nayakaribisha kwangu. Ni kitu ambacho sijakifanya, sijawahi kukifanya, ameniweka kwenye kundi ambalo mimi sipo, si mwanamke wa dizaini hiyo.

“Mtu anakwenda kwenye mkutano mkubwa kama ule mheshimiwa. rais anaufuatilia, badala ya kuongea mambo ya msingi yaliyotupeleka pale kama kutiana moyo na kuoneshana njia, wewe unaanza kuchambana, kwa kweli sikufurahia kwa sababu sijamsema popote, hata watu wanasema.  Mimi nimefundishwa nini niseme na mahali pa kusema, si kila sehemu unaweza kusema kila jambo.

“Nilijiuliza kwa nini ameamua kutengeneza jambo kama lile, nimemkosea nini mimi? Nikagundua kumbe Shishi ananichukia, lakini sijui ananichukia kwa lipi, sijawahi kujionyesha, mimi si mtu wa kujikweza, labda anaumia kwa vile ninavyopumua….. Sijawahi kuwa na matatizo naye huko nyuma, alishawahi kumwambia meneja wangu asinimeneji, lakini Mwenyezi Mungu ndiye hupanga kila kitu,” amesema Snura.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger