8/05/2020

Eymael Aigomea Adhabu ya TFF, Asema Aipo KisheriaALIYEKUWA kocha mkuu wa klabu ya soka ya Yanga, Luc Eymael amesema kuwa hakubaliani na adhabu iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kumfungia miaka miwili na kumtaka alipe faini ya Shilingi Milioni 8 kutokana na adhabu hiyo kukiuka taratibu za kisheria ikiwamo kutotoa nafasi ya yeye kujitetea.


 


Eymael hivi karibuni aliingia matatani baada ya kutoa kauli zilizotafsiriwa kuwa ni za kibaguzi baada ya mchezo wao dhidi ya Lipuli.


 


Akizungumza na Championi Jumatano kutokea nchini Ubelgiji, kocha Luc alisema taarifa za kufungiwa kwake hazijafikishwa kwa taarifa rasmi.
“Kwanza niseme kuwa sijapokea taarifa yoyote rasmi kutoka kwa uongozi wa Shirikisho la soka la Tanzania (TFF), kuhusu adhabu ya kunifungia na kulipa faini, hata mimi nimekuwa nikiziona taarifa hizo kupitia mitandao.


 


“Lakini suala jingine ambalo ndilo kubwa zaidi ni kwamba adhabu hii imetolewa bila kunipa nafasi ya kujitetea kitu ambacho kisheria ilikuwa haki yangu na wakili wangu aliwasilisha maombi hayo, hivyo kwa upande wangu nadhani adhabu hii ni batili na siwezi kukubaliana nayo,” alisema Eymael.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger