google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Familia yabariki Sure Boy kwenda yanga | UDAKU SPECIAL

Familia yabariki Sure Boy kwenda yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 BABA mzazi wa kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Abubakar Salum amesema ni muda muafaka kwa mwanaye kukipiga ndani ya kikosi cha Yanga ambayo imeonyesha nia ya kuitaka saini yake baada ya kuachana na viungo, Pappy Tshishimbi na Mohammed Issa ‘Banka’.

Mzazi huyo ameutaka uongozi wa Azam FC kumpatia mwanaye fursa ya kujiunga na Yanga kwani ni muda mwafaka kwa mchezaji na amekuwa akitamani kuichezea Yanga.

“Unajua hata Ulaya hakuna mchezaji ambaye hapendi kuchezea timu kubwa, kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani yeye kucheza Yanga, lakini pia ndani ya Azam amekuwa mchezaji mwandamizi kwa muda mrefu lakini amekuwa hapewi ile thamani yake kama mwandamizi, kwa upande wangu sina kipingamizi kuhusu yeye kujiunga na Yanga,” alisema Sure Boy.

Mabosi wa Yanga kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuhitaji saini ya Sure Boy na hivi karibuni waliwasilisha maombi ya kuhitaji kumnunua kiungo huyo ambaye amekuwa nembo ya Azam FC kwa miaka mingi.

“MaishaI ni kokote pale ambapo kuna mkate mnono ila kitu kikubwa zaidi cha kuzingatia ni nidhamu,” alimalizia mzee Aboubakar.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad