8/11/2020

Feisal Salum Aongeza Miaka Minne Yanga


Feisal Salum kiungo ndani ya Klabu ya Yanga kwa mujibu wa Injinia Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu hiyo amesema kuwa ameongeza mkataba wa miaka minne.

Kwa maana hiyo Feisal atakuwa ni mali ya Yanga mpaka 2024 kwa timu itakayokuwa inasaka saini yake lazima ijipange kuweka mkwanja mezani.

Kwa msimu wa 2019/20, Feisal amekuwa bora ndani ya Ligi Kuu Bara akianza kikosi cha Kwanza kwenye jumla ya mechi 22.

Ana tuzo ya mchezaji bora ndani ya Yanga aliyokabidhiwa na wadhamini wakuu wa Klabu hiyo, kampuni ya SportPesa.

Amefunga bao moja ndani ya ligi msimu huu ilikuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Mwadui FC kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger