8/30/2020

Gigy Money Amvua Nguo Mbwana Wake Mnigeria Hunchy Huncho


Dar: Siku chache baada ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kutengena na aliyekuwa bwana’ke, Hunchy Huncho ambaye ni raia wa nchini Nigeria, mazito yameibuka.


Kwa mara nyingine, Gigy amemvua nguo Huncho kwa kumwagia matusi kama yote. Gigy aliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa, watu wasidhani anaweza kurudi kwa Mnigeria na hamjui Mnigeria mmoja tu.


“Kama mnahisi namjua Mnigeria mmoja, poleni, eti Gigy amevaa hizi nguo amrudie Mnigeria, mimi huwa sirudi nyuma; yaani siwezi kula matapishi zaidi ya mara mbili, chunguzeni, yaani nisirudi kwa Ike wa Big Brother, nirudi kwa… (tusi la kumfananisha Huncho na mnyama).


“Kweli mtaniona mwehu, wazee waki-save screen shot, chukueni hii ya first lady (Mrs Ike Onyema Okwechukwu) drama queen,’’ aliandika Gigy anayedaiwa kuwa na tabia za ukorofiukorofi.

Stori: Happyness Masunga, Ijumaa
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger