8/22/2020

Guswa na Story ya Jackie Aliyejikuta Amekatwa Miguu Yote Miwili....Imechakatwa na ndugu yangu @malisa_gj

Kaka Malisa shikamoo. Naitwa Jacqueline Benn Munda nina umri wa miaka 21. Mwaka jana mwezi wa 7 nilianza kuumwa kichwa sana nikawa nazimia kila baada ya muda. Nilitibiwa hospitali mbalimbali kisha nikapewa rufaa ya kwenda Muhimbili. Baadae iligundulika nina ugonjwa unaojulikana kama Gregarine, na hivyo nilitakiwa kukatwa miguu.

Nilikataa kabisa na nilimwambia mzazi wangu anirudishe nikafie nyumbani. Nilirudi nyumbani Arusha lakini baadae nilipozidiwa mama alinipeleka hospitali ya KCMC ambako baada ya uchunguzi walisema natakiwa kukatwa miguu. Baada ya siku 13 za kukaa wodini nilikubali kukatwa. Haikuwa rahisi kukubaliana na hali hiyo hasa kutokana na ukweli kwamba nilizaliwa na miguu yote miwili na nilikua mzima wa afya.

Lakini namshukuru Mungu baada ya kukatwa miguu naendelea vizuti. Hitaji langu kwa sasa ni kupata miguu bandia ambayo inagharimu kiasi cha TZS 7M hapa KCMC. Kupitia wasamaria wema nimeshachangiwa kiasi cha 5.5M na hivyo kiasi kilichobaki ni 1.5M tu. Naomba unisaidie ili niweze kupata miguu bandia kaka yangu.

#MyTake:
Jacqueline anahitaji 1.5M tu ili apate miguu bandia. Angalau amekua mwaminifu kwa kuweka wazi kwamba ameshachangiwa 5.5M na wasamaria wengine. Asingekua mwaminifu angeweza kuficha hizo alizochangiwa kasema anahitaji 7M.

Naomba tumsaidie apate miguu bandia. Kiasi kilichobaki ni kidogo sana. Naamini ndani ya siku moja tunaweza kukamilisha, maana ukurasa huu umeshafanya maajabu kwa wengi.

Pichani ni Jacqueline alivyokuwa mwaka jana mwezi July na alivyo sasa. Yani ndani ya mwaka mmoja tu mfumo wa maisha yake yote umebadilika. Wahenga walisema hujafa hujaumbika. Leo kwa Jacqueline, kesho inaweza kuwa kwako.

Tuma mchango wako kwenda namba (MPESA) 0742 054 832 jina Mary Imbaseni Munda (mama mzazi wa Jacqueline). Kesho jioni tutahitimisha zoezi letu. Mungu akubariki sana.!
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger