Hakuna Upungufu wa Chanjo Tanzania -Dkt Subi Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa haina upungufu wa chanjo wa aina yeyote kwa watoto hivyo imewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto kuwapatia chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi amesema hayo wakati alipotembelea ghala ya kuhifadhia chanjo lililopo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

“tulikua na upungufu wa aina mbili za chanjo nchini kati ya tisa ambazo tumekuwa tukizitoa lakini, sasa hivi chanjo zote zipo, kwani zimeshawasili hapa nchini na usambazaji unaendelea”, amesema Dkt. Subi

Shule za serikali zatamba 10 bora kidato cha sita
Amesema kuwa, upungufu huo wa chanjo ulitokea baada ya Dunia kukumbwa na janga la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ambapo anga zote zilifungwa kwani chanjo husafirishwa kwa mnyororo baridi, kwahiyo huitaji usafiri wa anga.

“Tunamshukuru Rais  John Magufuli kwa kulifungua anga la Tanzania ambapo,  chanjo sasa zimeanza kuingia nchini na hadi sasa mikoa kumi na tatu(13) chanjo hizi zimeshapokelewa kati ya mikoa 26, na mikoa mingine kumi na tatu  ya Tanzania Bara usambazaji unaendelea kupitia Bohari ya Dawa (MSD)”.amesema Dkt. Subi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad