8/17/2020

Hatimaye Messi Aomba Kuondoka Barcelona



Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Lionel Messi, ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kuondoka kutafuta maisha mengine, huku Manchester City ikiwa ni timu pekee inayoonyesha shauku ya kutaka kumsajili.

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Esporte Interativo’ wa Hispania Messi, 33, anashinikiza kuondoka kutokana na matokeo mabaya yanayoikumbu timu hiyo.


Barcelona ilikula kichapo cha mabao 8-2 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka kwa Bayern Munchen.


Nyota huyo wa Argentina anayeaminika kuwa mmoja wa wachezaji wachezaji bora zaidi katika historia ya mchezo wa soka, ametumia muda wake wote akiwa na klabu hiyo yenye makao makuu yake Camp Nou kwa zaidi ya miaka kumi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger