8/18/2020

Hiki ndicho kikwazo cha Guardiola kurejea Barca


Wakala wa kocha Pep Guardiola ,ajulikanaye kwa jina la Maria Orobitig amesema mteja wake hawezi kuondoka Manchester City kwa sasa na ataendela kusalia na kikosi hicho kutoka jiji la Manchester.


Guardiola anatajwa huenda akawa Kocha mpya wa FC Barcelona kuchukua Mikoba ya Kocha wa sasa Quique Setién ambaye huenda akafutwa kazi muda wowote baada ya timu hiyo kutolewa kwa kipigo cha aibu cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Pep  amewahi kuifundisha Baracelona kati ya mwaka 2008 mpaka 2012 na alikiongoza kikosi hicho kushinda mataji 14 ikiwemo ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya UEFA champions League mara mbili.

Josep Maria Orobitig amesema kwa asilimia mia moja mteja wake atasalia katika klabu ya Manchester city na atamaliza mkataba  wa mwaka mmoja na Man City.

Makocha wengi wanaohusisha na Kibarua cha ukocha katika kikosi cha Barcelona ni Mauricio Pochettino, kiungo wa zamani wa kikosi hicho Xavi Hernandez,lakini hadi sasa taarifa zilizotufikia ni kwamba Ronald Koeman anakaribia kusaini mkataba wa kukifundisha kikosi hiko.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger