5/31/2022

Hivi Ndivyo Uzuri wa House Girl Ulivyomponza Mke wa MTU Mpaka Akaambukizwa Ukimwi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Inasikitisha sana. Fuatilia mkasa huu mwanzo mwisho....

Mke alimhisi mmewe kuwa anatembea na housegirl wao kutokana na ukweli kuwa, housegirl alikuwa mzuri mno kimuonekano, kiumbo na kwa sura. Alifikiri kumfukuza ila mme aligoma kutokana na uchapakazi wa binti yule. Hivyo, hakuona sababu ya msingi ya kumfukuza. Hakika housegirl alikua akizidi kumnyima usingizi mke wa boss. Kadri siku zilivyozidi kwenda, housegirl alizidi kumeremeta. Kila nguo aliyovaa ilimpendeza. Kila mkao aliokaa alionekana ni wa kimitego na hofu iliendelea kutanda kwa mke wa boss.

Mke alizidi kuhisi na mbaya zaidi kila siku usiku wakati mmewe akiaga kuwa anaenda kuangalia mpira sebuleni baada ya muda mfupi mke alikuwa anasikia miguno chumba mwa housegirl hivyo akajua itakua tu ni mmewe huwa ananyata na kumuingilia housegirl wao ndio maana mme shughuli chumbani siku za karibuni ilionekana kumshinda kwa kuchoka haraka mno.Jumamosi moja aliamua kumtuma housegirl kijijini kwa safari ya siku mbili bila kumjulisha mmewe wala mtu yeyote pale nyumbani. Usiku ule wa Jumamosi mme alimwambia mkewe utaratibu wake wa kawaida kuwa anaenda kuangalia mpira kwenye tv ya sebuleni. Kama kawaida, mke alikubali na mme akaenda sebuleni. Mke taratibu aliingia chumbani kwa housegirl akajilaza kitandani uchi kama alivyozaliwa. Kama kawaida alisikia mlango ukifunguliwa taratibu akaingia mtu akapanda kitandani na bila kuuliza akavua nguo akaanza kula tunda. Baada ya goli la 5, mke alisema, *_"INATOSHA. LEO NIMEKUKAMATA. KUMBE HIVI NDIVYO HUWA UNAFANYA NA HOUSEGIRL WAKATI UKIWA NA MIMI GOLI MBILI TU UNASEMA UMECHOKA? MCHEZO WAKO HUU NDIYO UNAKUMALIZA NGUVU NA UKIJA CHUMBANI KWANGU UNASEMA UMECHOKA WAKATI HAPA TAYARI MABAO MATANO NA UNATAKA UENDELEE?_*"

Kwa MSHTUKO, ghafla mme alijibu, "SAMAHANI mke wa boss sikujua kama ni wewe. Mimi ni houseboy wenu mkata majani; nisamehe tafadhali!"


Mke alishtuka akapiga kelele kwa kupaniki maana alimjua houseboy wao alivyo mwathirika hata kumuajiri pale kwao ilikuwa ni kwa kumsaidia maana yeye na mme wake wanamjua ni kijana yatima aliyekuwa amezaliwa na UKIMWI kwani wazazi wake walipofariki alitengwa na ndugu ndipo wakamsaidia wakamuajiri kuwa houseboy wao ili akate majani, kuzibua vyoo n.k.

Kelele alizopiga mama zilimkurupusha mmewe sebuleni na kuwasha taa za nyumba nzima kisha akaelekea chumba cha housegirl kujua nini kimemsibu mkewe. Alipoingia hakuamini macho yake kwa kumwona MKEWE AKIWA UCHI WA MNYAMA KITANDANI NA HOUSEBOY WAO AKIMBEMBELEZA UCHI KAMA WALIVYOZALIWA.

*_WIVU MBAYA JAMANI!!!_*

Ama kweli umdhaniaye ndie siye, na usilolijua ni usiku wa giza. Maskini mama mwenye nyumba kajiponza kisa wivu. Alijua mmewe anatembea na housegirl kumbe baba wa watu hana shida na mtu yuko busy na mambo yake. 


Sasa yamemkuta makubwa mama huyu aibu hii atamuelewa nani mbaya zaidi houseboy ni mwathirika. Je, kama ameambukizwa UKIMWI itakuwaje? Hakika, familia na nyumba nzima imekumbwa na giza nene. NAAMINI WENYE TABIA ZA KUHISI NA KUAMINI TETESI BILA KUTHIBITISHA MTAKUA MMEJIFUNZA KITU.

JE! UNGEMSHAURI MME ACHUKUE MAAMUZI GANI?

Usiku mwema na Mungu awabariki na kuwalinda!!!


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

4 comments:

 1. Asimuache kwani huo wrote ilikuwa ni wivu Wa kumpenda mumewe,ila kajaliwa hivyo .subiri mpaka miezi 6 kisha ampeleke akapimwe.

  ReplyDelete
 2. ampeleke hospitali kwani kuna dawa ya kuzuia kuambukizwa ndani ya masaa 36,

  ReplyDelete
 3. HADITHI HISIO KWELI .HUWEZI KUVAA KIATU KISICHOKUA CHAKO BILA KUJUA KWA MUDA MREFU.
  HUYO MWANAMKE AMEINGILIWA NA HOUSEBOY MPAKA ROUND YA TANO BILA KUJUA MIPIGO SIO YA MUMEWE?NA HARUFU YA MUMEWE PIA HAIJUI?

  ReplyDelete
 4. hapana kuna tatizo katika hii habari, kwanza haiwezekani asijue analala na nani pili angeendelea kumchunguza mume wake ukweli angeupata .

  ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger