8/13/2020

Humud asaini mkataba wa miaka miwili Namungo FC


ABDULHALIM Humud aliyekuwa kiungo wa Mtibwa Sugar leo Agosti 13 amekamilisha dili la kujiunga na Namungo FC iliyo chini ya Hitimana Thiery.


Humud aliyekuwa anatajwa kuibukia Yanga msimu wa 2020/21 amesaini dili la miaka miwili ndani ya kikosi cha Namungo FC.Akiwa Mtibwa Sugar, msimu wa 2019/20 alihusika kwenye jumla ya mabao mawili kati ya 30 ambapo alifunga mabao mawili ndani ya kikosi hicho.Atakuwa kwenye kikosi kitakachoipeperusha nchi kimataifa msimu ujao kwenye Kombe la Shirikisho.Namungo FC itashiriki michuano ya Kimataifa baada ya kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho na kucheza na Mabingwa wa Ligi Kuu Bara ambao ni Simba.Licha ya kuwa walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 nafasi ni yao kwa kuwa Simba ataiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.Kiungo huyo aliwahi kukipiga ndai ya Simba na KMC.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger