8/27/2020

Idris Sultan aingia rasmi kwenye muzikiMchekeshaji na muigizaji wenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram Idris Sultan amehamia kwenye fani nyingine ya kuimba baada ya kushirikishwa kwenye remix ya wimbo wa msanii Motra The Future "masihara". 


Mshindi huyo wa mashindano ya Big Brother Africa miaka iliyopita, ameonekana kwenye picha na video wakiwa location na mmiliki wa wimbo baadhi ya mistari aliyoiimba ndani ya wimbo huo inasomeka kama ifuatavyo. 


"Nimerudi na natesa uko wapi wewe ambaye ulikuwa unateta, ulitabiri huu ndiyo mwisho wangu wa kusepa, nikiwepo unacheka nikiondoka unaniteta kiti changu hakikaliwi na viatu vya havivaliwi hasa kwa wewe bishoo ambaye hung'ai bila kiwi, hiki kipara sikupewa kama ni pambo acha nifunge magoli yangu usinipangie kiwango" ameimba Idris Sultan 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger