IGP aonya vyama kuingilia majukumu ya Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni za amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi na baada ya Uchaguzi kwa kile alichodai kuwa kuna maisha baada ya Uchaguzi hivyo hawatakiwi kuvunja amani.


IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo Agosti 19 katika mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi pamoja na vyama vya siasa, ambao ametaka kila mtu atimize wajibu wake, na kuonya vyama kutoingilia majukumu ya Jeshi la Polisi.

"Msiingilie kazi ambazo sio zenu, baadhi ya wagombea kutangaza dhana ya kulinda kura ambayo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu", ameesma IGP Sirro.

IGP Sirro ameongeza kuwa, “Tuko vizuri sana kushughulika na wahalifu, mwanasiasa akijiingiza kwenye uhalifu basi huyo ni halali yetu, hakikisheni mnafanya siasa safi za amani na utulivu”.

Mkutano huo wa Tume, Vyama vya siasa na wadau wa Uchaguzi, umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama, vyama vya siasa na viongozi wa Dini mbalimbali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad