8/08/2020

India: Kisanduku cheusi chapatikanaMkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la India Express ambalo ndege yake ilipata ajali kwenye jimbo la kusini mwa India ameliambia shirika la habari la Reuters leo Jumamosi kwamba kisanduku cheusi cha kunakili taarifa za safari ya ndege kimepatikana. 

Ndege hiyo ilikuwa ikiwarudisha raia wa India waliokuwa wamekwama Dubai tangu kuanza mlipuko wa COVID-19, iliteleza na kupitiliza barabara ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kalicut kutokana na mvua kubwa karibu mji huo wa kusini mwa India wa Kozhikode hapo jana Ijumaa. 


idadi ya vifo imeongezeka na kufikia watu 18. Watu wengine 16 walijeruhiwa vibaya kwenye ajali hiyo. Maporomoko ya udongo na mafuriko ni jambo la kawaida wakati wa msimu wa mvua kubwa zinazonyesha kati ya miezi ya Juni na Septemba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger