8/07/2020

Jamaa Amuuza Mkewe kwa Mpango wa Kando baada ya Kumnasa Peupe Wakilabishana AsaliWatendaji Mbozi wadaiwa kutafuna Sh260milioni - Mwananchi

Jamaa huyo alimfumania mkewe akilishwa uroda na mume asiyemjua

Aliwaacha wengi vinywa wazi akitaka malipo ya TSh 100,000 ili kumwachia mke huyo

Jamaa mmoja mwenyeji wa eneo la Njukuni, kaunti ya Taita Taveta aliwaacha wengi vinywa wazi kutokana na hatua aliyoichukua baada ya kumfumania mkewe akihusika katika tendo la ndoa na mpango wa kando.

Kulingana na jarida la Taifa Leo, mume huyo alipashwa habari kuwa kuna jamaa aliyekuwa akimsaidia kuchovya asali ya mkewe ndipo akaamua kufanya upekuzi wake.

Siku ya kisa, bwana huyo alifanya mpango na kuwafumania wawili hao peupe wakipokezana mabusu. Bwana huyo hakushangaa.Alimwambia huyo bwana kuwa atamwachia mke huyo bora amlipe TSh 100,000 ili asiwe na shida ya kujificha tena wakifanya mahaba.

Bwana huyo alitishia kuwa iwapo jamaa huyo angekataa kulipa, angemuaibisha zaidi na kumsababishia majeraha mabaya.

Bwana huyo ambaye hakuwa na lolote lingine la kufanya alilazimika kutoa hela hizo na kumkabidhi mume huyo upesi kabla  kuuita umma.

Bwana huyo alimshukuru na kuwatakia maisha marefu na kuenda zake bila kujali mkewe tena.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger