8/09/2020

Jaydee Amtaja Msanii Asiyetaka Kumkosa Jukwaani Katika Tamasha Lake


Msanii nguli wa Bongo Fleva Lady Jaydee amesema kuwa hayuko tayari kumkosa msanii mwenzake mkongwe Professor Jay katika tamasha lake la 'Miaka 20 ya Lady Jaydee'.

Amesema hayo katika mahojiano na Rais wa Bongo Fleva, Dullah Planet katika Friday Night Live ya EATV, ambapo amesema kuwa yuko tayari awakose wasanii wengine lakini siyo Professor Jay kwakuwa ni mtu wake tangu zamani na anamuamini.

"Tamasha langu la miaka 20 ya Lady Jaydee lilisimama miezi yan katibuni kutokana na Corona na tulishaanza mwezi wa tatu lakini sasa hivi tutatoa ratiba na wasanii watakaokuwepo kwenye urejeo wangu", amesema Jaydee.

"Lakini mwezi huu wa 8 tutarejea na tutatoa taarifa lakini nisingependa kumkosa Professor Jay nimeshasema kwenye TV, yaani nitamuomba hata siku moja aje. Ni mtu wangu sana katika miaka 20 ningependa yeye aje", ameongeza Lady Jaydee.

Lady Jaydee ametambulisha wimbo mpya unaojulikana kwa jina la 'Ni Hapo' ambao amemshirikisha Joh Makini.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger