8/27/2020

Jeff Bezos Aweka Rekodi ya Dunia Amekuwa Mtu wa Kwanza Kuwa na Utajiri wa $200B

Uko wapi ndugu yangu? Kama umekaa kizembe muda huu basi fahamu kwamba Jeff Bezos ameandika rekodi ya dunia kwa kuwa mtu wa kwanza kufikisha utajiri wa ($200 Billion)

Usiku wa kuamkia leo Jarida la Forbes limemtaja Bezos ambaye ni mwanzilishi wa kampuni ya Amazon kuwa amefikisha utajiri wa ($204 Billion) hivyo kumfanya kuwa mtu wa kwanza kuwa na utajiri huo wa fedha. Soko la hisa la Amazon limepaa kwa asilimia 2 jana mchana na kutengeneza kiasi cha $4.9 Bilioni.

Kwa sasa amekalia namba 1 kwenye orodha ya matajiri wa dunia akiwa na utajiri wa ($204.6 Billion) sawa na TSH. Trilioni 473, akimuacha Bill Gates kwa kiasi cha ($90 Billion) Gates kwa sasa ana utajiri wa ($116.1 Billion)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger