8/13/2020

JPM Amsamehe Mkurugenzi Ikwiriri Aliyedanganya Gari ni BovuPwani : 

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amemsamehe Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rufiji, Brighton Eliud Kilimba, aliyetoa taarifa za uongo kuwa gari la Kituo cha Afya Ikwiriri haliwezi kutembea wakati akizungumza na wananchi alipopita Ikwiriri Rufiji mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa mkoa wa kipolisi Rufiji, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Onesmo Lyanga amesema uchunguzi ulifanyika kwa gari lenye namba za usajili STL 940 aina ya T/land Cruiser la Kituo cha Afya Ikwiriri, limegundulika lina uwezo wa kutembea na siyo kama taarifa aliyotoa kaimu mkurugenzi kuwa ni bovu.

“Tulimkamata tarehe 01.08.2020 kwa kosa la kutoa taarifa ya uongo na utaratibu wa kumfikisha mahakamani kwa kosa hilo ulikuwa unakamilishwa, leo amepata bahati, rais ameamua kumsamehe na kwasasa yuko huru,” Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Onesmo Lyanga
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger