8/27/2020

Kampuni za ndege za Kenya zazuiwa kuingiza ndege zake Tanzania
Fly540 ni moja ya makampuni ya ndege ya Kenya yaliyozuiwa kuingia TanzaniaImage caption: Fly540 ni moja ya makampuni ya ndege ya Kenya yaliyozuiwa kuingia Tanzania


Kampuni tatu za ndege za Kenya zimezuiwa kuingia nchini Tanzania kufuatia hatua za kudhibiti janga la korona. Mamlaka ya anga ya Tanzania imezizuwia kampuni za AirKenya, Fly540 na Safarilink Aviation zote kutoka Nairobi.


Mkurugenzi wa TCAA, Hamza Johari amethibitisha katika mahojiano na gazeti la Citizen nchini humo. Nchi hizi mbili za Afrika Mashariki zipo kwenye mzozo wa kutokukubaliana juu ya namna zinavyokabiliana na janga la virusi vya corona.


Mwezi huu Kenya ilitangaza ilitoa orodha ya nchi 130 ambazo wasafiri wake hawatawekwa karantini watakapoingia nchini Kenya.Tanzania haikuwemo.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger