Kikongwe wa Miaka 74 Anaswa Airport Akisafirisha Mabaki ya Mumewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Polisi katika uwanja wa ndege wa Munich nchini Ujerumani wamepigwa na mshangao mkubwa wakati wakichunguza sanduku la mbao lililokuwa linasafirishwa na abiria mmoja kikongwe mwenye umri wa miaka 74 ambalo waligundua kuwa lina mifupa ya mume wa mama huyo, maafisa wamesema hapo jana Jumanne.

Maafisa wa forodha, daktari na waendesha mashitaka waliitwa, na kugundua kuwa hakuna uhalifu uliofanyika, shirika la habari la Ujerumani DPA limeripoti.


Baada ya kumhoji mwanamke huyo na mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 52, polisi iligundua kuwa wanawake hao wawili walikuwa safarini kutoka Ugiriki kwenda katika nchi walikozaliwa ya Armenia kupitia Munich na Kiev.

Polisi wamesema Mama huyo alisema mume wake alifariki mwaka 2008 na alizikwa mjini Thessaloniki, Ugiriki na kwamba yeye na mtoto wake wa kike waliamua kurejesha mabaki hayo nyumbani nchini Armenia.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad