8/01/2020

Kim Kardashian Atokwa na Machozi Baada ya Kukutana na Mumewe Kanye West

Kim Kardashian asafiri na kukutana na mumewe Kanye West, makutano yao ya kuiweka sawa ndoa yao, yalitawaliwa na majonzi ambapo Kim alionekana akitokwa na machozi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TMZ, Jumatatu (July 27) ilikuwa ndio mara ya kwanza kwa wao kukutana tangu kauli tata za Kanye West ambazo alizitoa kwenye ufunguzi wa kampeni zake mjini South Carolina. Kanye alitoa kauli tata ikiwemo ya kuwahi kutaka kuutoa ujauzito uliokuwa umembeba binti yake, North West, kauli ambayo ilimuumiza Kim na kumfanya Kanye kuomba radhi kupitia twitter.

Kauli zingine za Kanye ni ile ya kutaka kupeana talaka mara baada ya kumtuhumu Kim kuwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Meek Mill, kauli ambayo iliteteresha ndoa yao.

Kwenye mfululizo wa picha zilizotolewa na TMZ, wawili hao walionekana kwenye gari wakienda kupata chakula pamoja mjini Wyoming.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger