Kimbunga Laura chatua Louisiana, Marekani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kimbunga Laura kimefika katika jimbo la Louisiana nchini Marekani mapema leo na kuwa ni kimbunga hatari sana kilicho katika kiwango cha nne.


Kimbunga hicho kiliingia katika jimbo hilo la Louisiana, kiasi cha kilometa 220 Mashariki mwa Houston, Texas, kwa mujibu wa kituo cha taifa cha uchunguzi wa vimbunga, ambacho hapo kabla kilitoa tahadhari kwamba kimbunga hicho kitakuwa kikubwa sana na kutoweza kuhimilika.


Upepo unaonekana kuwa na kasi ya kiasi cha kilometa 240 kwa saa, licha ya kuwa mawimbi yanaweza kupita kiwango hicho.



Zaidi ya watu 500,000 wamewekwa katika amri ya kuondolewa katika sehemu za Texas na Louisiana wakati kimbunga hicho Laura kikielekea katika pwani ya ghuba ya Marekani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad