8/11/2020

Kinachojiri Sakata La Morrison TFF, Mwana FA Atoa Ya Moyoni


Ikiwa bado kikao cha kamati ya maadili na nidhamu cha shirikisho la soka nchini (TFF) kikiwa kinaendelea kusikiliza shauri la utata wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Bernard Morrison mwanamuziki Hamis Mwijuma (Mwana FA) ambaye ni shabiki wa Simba SC amepenyeza taarifa za ndani juu ya kinachoendelea kwenye kikao hicho.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Mwana FA amedokeza kuwa, Mahasimu wao Yanga wameshinda shauri hilo na Morrison ni mchezaji wao halali.

“Kwa hivo Yanga wameshinda shauri na Morrison ni mchezaji wao halali..kwa hivo kimsingi wana Morrison na Senzo, enhe tunajiteteaje wazee wangu ?” Amendika Mwana FA.

Morrison alitangazwa kujiunga na klabu ya Simba siku chache zilizopita baada ya kuwa na mgogoro wa  muda na klabu yake ya Yanga
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger