8/11/2020

Kisa Bangi, Harmonize Hajanisalimia kwa Miaka 3 – Sallam SKMENEJA wa Kimataifa wa Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Sallam SK kutoka lebo ya WCB, ameamua kuweka wazi bifu lililopo kati yake na msanii Harmonize, ambaye aliwahi kuwa msanii chini ya lebo hiyo inayosimamiwa na Diamond.

Sallam amesema kuwa tofauti kati yake na Harmonize ilianza muda mrefu tangu miaka mitatu iliyopita, baada ya Harmonize kumtuhumu yeye na Babu Tale kuwa ndio waliopeleka taarifa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba Harmonize anavuta bangi.

Sallam ameeleza kwamba tangu kipindi hicho, Harmonize hakuwahi kumsalimia na alikuwa akimpita kama jiwe mpaka siku ya msiba wa mke wa Babu Tale ambapo alimsalimia Sallam lakini naye aliukataa mkono wa msanii huyo.

“Mimi sio mnafiki, kama mtu aliamua kutonisalimia na mara nyingi amekuwa akinikataa kwa zaidi ya miaka mitatu sasa..kuna haja gani ya kusalimiana naye. Ndio maana hata ule mkono alionipa niliukataa…” Aliongeza Sallam akifafanua kuhusu ile ‘issue’ ya kuukataa mkono wa Harmonize kwenye msiba wa mke wa Babu Tale.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger