8/07/2020

Kisa cha Mama Aliyemchoma Mwanawe kwa Kuiba Chapati Zake Mbili


Mama huyo wa umri wa miaka 38 aliwashangaza wengi kwa hatua ya kumchoma mwanawe

Mtoto huyo ambaye alitambulika kama Brian ni mwanafunzi wa darasa la pili

Babuye mtoto huyo alisimulia jinsi alivyompata Brian kwa uchungu mwingi

Mama mmoja mwenye umri wa miaka 38 sasa atalazimika kusalia korokoroni baada ya kumchoma mwanawe wa kiume kwa tuhuma za kuiba chapati zake.

Kulingana na mdaku wetu, mama huyo anadaiwa kuchukua mafuta na kumwagia mwanawe kabla kumchoma akidai kuwa mtoto huyo alikula chapati zake mbili bila idhini.

Katika kisa hicho kilichofanyika eneo la Matere, Lugari katika kaunti ya Kakamega, inadawa kuwa mama huyo alimuamuru mtoto huyo wa darasa la pili kuvua nguo zake zote kabla kumtekelezea unyama huo.

Kenyan police killed by roadside bomb in Garissa near Somalia border

Mama huyo alikamatwa na polisi. Picha: Hisani

Akisimulia kisa hicho, Jackton Shikuku bubuye Brian alieleza kuwa alimpata mtoto huyo akilia kwa uchungu mkubwa, na kumweleze jinsi mamake alivyomchoma kwa mafuta kwa kula chapati mbili.

Aidha alieleza kuwa mama huyo alikuwa akimtunza mtoto huyo visivyo, kulingana naye, mama huyo amekuwa akimtelekeza mwanawe huyo,sababu ikikosa kubainika.

Polisi walipata habari kuhusu kisa hicho na kumkamata mama huyo na kumtia korokoroni kusubiri kufikishwa mahakamni kufunguliwa mashtaka.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger