8/26/2020

Klopp: Ubingwa wa Bayern ‘Ni Bahati Tu’Klopp anajiandaa kuvaana na Arsenal kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kupigwa Jumapili hii katika dimba la Wembley, saa 12:30 jioni.

kocha wa Liverpool Mjerumani, Jurgen Klopp amesema kuwa kitendo cha Bayern Munich kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ilikuwa ni bahati na ilisaidiwa zaidi na ratiba yake.

Klopp ambaye amewahi kuwa mpinzani mkubwa wa miamba hiyo wakati anahudumu Borussia Dortmund kuanzia mwaka 2008 hadi 2015, ameanza kwa kuwapongeza kwa ubingwa huo lakini hakuacha kutoa mtazamo wake.

“Bayern walikuwa na bahati na hiyo ilitokana na aina ya ratiba yao ambayo ilikuwa inawafanya kuwa bora kwenye UEFA, ukiacha hilo pia imekuwa ni kipindi ambacho wana timu bora na nzuri ambayo inajengwa na wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa,” alisema.

Klopp alikuwa anazungumzia ratiba kama chanzo cha Bayern kufanya vizuri kwani Ligi Kuu ya Ujerumani ndio ilikuwa ya kwanza kurejea mwezi Mei, baada ya ligi kusimamishwa kwa hofu ya janga la Corona, hivyo Bayern ilimaliza ligi wakati timu pinzani ilizokuwa inacheza nao bado zilikuwa na ratiba ya ligi na Uefa huku yenyewe ikiwa na ratiba moja tu.

Inaaminika kuwa jambo hilo liliifanya Bayern kuwa na muda mwingi wa kupumzika na kufanya mazoezi tofauti na wapinzani wake na mfano ni kwa PSG ambayo ligi haikurejea kabisa hivyo haikuwa.

Klopp anajiandaa kuvaana na Arsenal kwenye mechezo wa ngao ya Jamii unaotarajiwa kupigwa Jumapili hii katika dimba la Wembley, majira ya saa 12:30 jioni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger