8/26/2020

Kocha Kaamua! Suarez, Vidal, Umtiti, Rakitic Out BarcelonaTAARIFA za kuachwa kwa mastaa wa soka wa timu ya Barcelona ya Hispania  zimetolewa na vyombo vya habari nchini humo  siku kadhaa baada ya Ronald Koeman kutangazwa rasmi kuwa kocha wa miamba hiyo, ambapo atahudumu hadi mwaka 2022.

Taarifa zinadai kuwa huyo kocha mpya,  amewasiliana na wachezaji wake wanne Luis Suarez, Ivan Rakitic, Arturo Vidal na Samuel Umtiti kuwa wapo huru kuondoka katika dirisha hili la usajili.

Kitendo hicho kinatajwa kuwa huenda kikaigharimu Barca mpunga mrefu ikiwa hakuna timu ambayo itawasilisha ofa za kuwasajili, jambo ambalo litawafanya wavunje mikataba yao, kwa kuwa wachezaji wote hao bado wana mikataba na Umtiti ndiye ana mkataba mrefu zaidi unaomalizika mwaka 2023.

Upande wa Luis Suarez mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2021, na pia ni miongoni mwa wachezaji ambao wanakunja mpunga mrefu, ambapo kwa wiki anachukua jumla ya Pauni milioni 3,  hivyo ikiwa itavunja mkataba wake itahitajika kumlipa sio chini ya Pauni 12 milioni.

Pia, Arturo Vidal naye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2021, huku na yeye akiwa anabeba jumla ya Euro milioni 1 kwa wiki na ikiwa hakuna klabu ambayo itahitaji huduma yake, Barca italazimika kuvunja mkataba wake na kumlipa pesa zake zilizobaki.

Mwamba mwengine ambaye ameonyeshwa mlango wa kutokea ni Ivan Rakitic ambaye naye pia mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2021, na anachukua Pauni milioni 2  kwa wiki. Kwa jumla pesa ambayo itaitoa kuvunja mikataba yao ni zaidi ya Pauni milioni 60.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger