5/30/2022

Komaa na Akaunti Yako...Soma Kisa Cha JAY Z Kudharauliwa Hadi Kuja Kuwa Bilionea

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA
UNATAZAMA wenzako, unajiona upo nyuma sana. Watu wa umri wako maisha yao ni tambarare. Watoto wadogo wapo vema. Wewe maisha hayana uhakika.

Kisa cha Dengule kujinyonga ni mawazo kama hayo. Alijiona kaachwa nyuma sana kimaisha, halafu kila anachokifanya hakiendi. Akajitundika kambani. Mungu amsamehe dhambi zake.

Mwaka 1995, Jay Z angewaza kama Dengule. Majanki wenye umri wake na madogo kwake walikuwa wana-ball kwenye muziki Marekani. Wanatengeneza fedha na kuishi maisha yao to the fullest.

Schoolmates wake, Notorious BIG na AZ walikuwa wakiogelea utajiri. Wakati huo, Jay Z kila lebo aliyokwenda kuomba imsaini, ilimkataa. Washika dau hawakuona hela ndani yake.

Jay Z alikuwa pusha wa dawa za kulevya tangu akiwa na miaka 10. Mtoto m'bad wa Brooklyn, mitaa yenye viatu vilivyoning'inizwa kwenye nyaya za umeme, alitaka kuachana na hiyo mitikasi ya ngada na kukimbizana na manjagu ili aishi kama staa na tajiri.

Pusha mwenzake, BIG, alishaacha michongo hiyo na tayari albamu yake "Ready to Die" ilikuwa inaua sana sokoni.

Wakati huo soko la Hip Hop lilikuwa likimilikiwa na makachaa wa West Coast. Akina Tupac Shakur, Snoop Dogg na wengine. Waliovimba East Coast ndio hao akina BIG, Mobb Deep, Nas na wengine ambao kwa umri walikuwa madogo kwa Jigga.

Jay Z alikuwa na kigari chake alichonunua kwa pesa za unga. Akawa anauza CD za nyimbo zake kama mmachinga. Washikaji zake, Dame Dash na Kareem Burke, wakamwambia waanzishe lebo yao. Roc-A-Fella Records ikazaliwa.

Kwa pesa za kuungaunga, Jigga akatoa albamu ya kwanza "Reasonable Doubt". Kwa sababu ya kutokuwa na msuli mzuri wa kuitangaza, ilibidi waachie nyimbo nyingi mfululizo ili zitumike kuinadi albamu. Mwisho, Reasonable Doubt iligonga platinum.

Wakati wa kutengeneza albamu, Jigga aliwaalika washkaji zake, Nas na AZ wampe tafu kwenye wimbo "Dead Presidents", walimchomolea. Walimuona underground.

Kilichofuata, Jigga akawa supastaa tajiri. Ilipofika mwaka 2019, Forbes walimtangaza kuwa bilionea wa kwanza wa Hip Hop kwa sarafu ya The Fed. Trilionea wa shilingi.

Usikonde kwa mafanikio ya mapema waliyonayo wenzio. Komaa na akaunti yako. Piga kazi. Usikate tamaa. Kama Jigga.

Ndimi Luqman MALOTO
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger