8/29/2020

Kumbe Mwigiza wa Black Panther Aliyefariki Aliigiza Black Panther Akiwa Mgonjwa...Inasikitisha Sana

Tuzidi kumshukuru Mungu matatizo hayajiandiki usoni, huyu kaka aliumwa Kansa ya Utumbo mkubwa kwa miaka minne. Ni muda huu huu pia ameigiza movie ya Black Panther maarufu kama Wakanda na nyingine nyingi.

Hapo nyuma kuna picha na video zake zilisambaa akiwa amekonda na kudhoofu sana. Kuna waliosema anatumia madawa ya kulevya na wengine wakasema anajikondesha. Alisemewa vitu vibaya, kibinadamu ingekuwa nafasi yake ya kuitangazia dunia kujitetea kuhusu maradhi yake yaliyokuwa yakimtesa. Aliamua kuugulia kimya kimya mpaka mauti kumkuta.

ia tusiyojua, usiwe sehemu ya nyongeza ya maumivu. Nikukumbushe pia kuishi kwa ukamilifu, ukijitoa na kujisukuma kufanikisha unayoweza. Kama aliigiza kama King Tchalla, nafasi iliyomuhitaji kimwili kwa mazoezi magumu na kiakili kuzingatia mistari na uigizaji, akiwa mgonjwa wa Kansa, sisi tulio wazima, tuna kisingizio gani? Mungu atusaidie #RIP #WakandaForever
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger