8/07/2020

Kwanini Ufie Hapo? Wacha Kumsingizia Mungu Kwa Kila Shida Unayopata....Pambana na Hali yako Utoke

KWA NINI UFIE HAPO?
Kama kuna watu ninaowahurumia ni wale ambao kila shida, jaribu, tatizo ama changamoto wanayopitia wanabaki kusema ni mapenzi ya Mungu, na wala hawachukui hatua yeyote ya kupambana kiimani ili kutoka hapo.
SIKILIZA..
Hakuna jaribu, shida, wala tatizo unalostahili kulipa heshima na hadhi ya "mapenzi ya Mungu" ikiwa lipo kinyume na Neno la Mungu. Vinginevyo, Shetani ataendelea kukuchezea for good na anaweza kuua furaha yako, kuua uchumi wako, na hata kuwaua wapendwa wako ama wewe mwenyewe kabla ya wakati wao.

CANT YOU SEE?
Umechelewa kupata mtoto ama mimba zimekua zikiharibika, halafu unapigwa chenga kuamini kwamba ni mapenzi ya Mungu, ilhali unajua kabisa Neno linasema "Hakuna atakaekua tasa wala mwenye kuharibu mimba".(KUTOKA 23:26) Whaaaat!??? Huyo ni shetani, inuka upiganie haki yako.
Madeni yamekuzidia, bado unaenda kukopa zaidi ili uwalipe wale wanaosumbua, halafu unajisemea na kuamini kwamba ni mapenzi ya Mungu? Kivipi? Neno linasema, anaekopa ni mtumwa wa anaekopesha. (MITHALI 22:7). Mungu anaanzaje kukutia utumwani? Huyo ni shetani anacheza na mindset yako kuhusu mikopo na madeni!
Umeugua ama umeuguza muda mrefu halafu mtu anatokea from no where anakuambia vumilia tu kwa sababu ni mapenzi ya Mungu na wewe unaamini? How? Ina maana hujui kwamba Neno linasema unatakiwa uishi maisha marefu yenye amani, uzima na furaha? (MITHALI 3:2). Sometime shetani analeta magonjwa kwako wewe ama kwa wanaokutegemea, ili uwe bize mahospitalini na mambo mengine yaparaganyike. Stand up and fight in faith!

NIKWAMBIE KITU?
Shetani na Mungu huwa hawatendi lolote maishani mwako pasipo ruhusa yako. Shetani anasubiri uende kinyume na Neno (ukate tamaa) ili atekeleze yake. Mungu anasubiri usimame katika Neno ili atimize mpango wake. Be careful!

HOPE UNAKUMBUKA.....
Namna shetani alivyonijia ili kupata ruhusa yangu ili amuue mke wangu alipokua akijifungua hawa mapacha wa pili(Nathan na Nathanael). Kilichoniokoa ilikua ni kusimama katika Neno na kujibizana nae strongly. Mind you kwamba, kumshinda Shetani kunahitaji "ungangari" wako katika Neno na katika Imani, vinginevyo, you will always be a cheap prey of a devil!
Mke wangu akiwa kaingia theatre, shetani akaniambia "Albert umeshafeli kiimani! Kwa nini umeruhusu mke wako afanyiwe oparesheni ya uzazi? Oparesheni sio mpango wa Mungu na katika oparesheni wanawake wengi huwa wanakufa wao ama watoto wanaozaliwa". Shetani alitaka nikubaliane nae ili nisiendelee kuomba na nibaki nasubiri patapotea ya eidha mke kutoka mzima ama akiwa maiti. Nikamwambia, Shetani acha kunitisha, oparesheni ya uzazi sio jambo jipya kwa Mungu kwa sababu ipo katika, ISAYA 66:7. Shetani aliponisikia hivyo akanywea!
Lilipotokea tatizo la kuishiwa damu, Shetani akaniambia mke wangu atakufa kwa sababu ya kukosa damu. Nami chapchap nikamjibu na kumwambia, Yesu Kristo ana damu nyingi hadi aliimwaga chini, kwa hiyo haiwezekani Yesu awe ndani yangu na ndani ya mke wangu halafu damu iwe ni tatizo.
(MATHAYO 26:28).
Aliponiletea picha ya jeneza likiwa na mwili wa mke wangu, nikamwambia, shetani unapoteza muda kwa sababu Neno linasema nitamfurahia mke wa ujana wangu hata niwapo mzee, kwa hiyo siwezi kuzika mke katika ujana huu.(MITHALI 5:8, ZABURI 92:14). Kwa masaa karibu manne (saa saba usiku hadi saa 11 nilikua nikipambana na shetani, aliekua akitafuta ruhusa yangu amuondoe mke wangu. Alinisemesha na kunionesha mengi nami nilimjibu kwa Neno hatua kwa hatua. Hatimae nilimshinda na akaondoka akiwa ameaibika na kuacha Mungu akijitwalia utukufu (YAKOBO 4:7)

NAKUSHAURI USIFIE HAPO..!!
Kuanzia dakika hii, achana na habari ya kuvumilia shida, jaribu ama tatizo lako kwa kujifariji kuwa ni mapenzi ya Mungu. No! No! No! Hebu inuka, jikung'ute, acha kujikunyata, funga ngumi za kiimani, pigania haki yako iliyopo katika Neno inayohusiana na jaribu, shida ama tatizo linalokuliza na kukuhuzunisha kila siku. Maandiko yanasema Ufalme wa Mungu unatekwa kwa nguvu, tafadhali usiende kama kondoo bali simama na upambane kama simba tena kwa nguvu zote. (MATHAYO 11:12) #SmartMind
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger