8/01/2020

Lulu Diva afunguka bifu lake na NandyMsanii wa muziki wa kibongo Lulu Diva amesema ugomvi unaodaiwa ulikuwepo kati yake na msanii mwenzake Nandy ni wa kitoto tu. 


Lulu Diva ambaye yupo Jijini Mbeya hivi sasa alipoenda kwenye Show ya "Gigy ni Kiki" Home Coming iliyoandaliwa na Swahili Flix, amesema siku zote panapo kuwepo wanawake zaidi ya wawili, hakukosekani maneno ya hapa na pale, hivyo ndiyo maana kukatokea ‘kaugomvi’ ambako hata hakakuwa na msingi wowote.


“Sidhani kama nilikuwa na ugomvi wa maana kati yangu na Nandy, yaani ni ugomvi tu wa ki-mwanamke, hauna maana yoyote na pia hakuna kitu kibaya kama maneno ya kuambiwa, hivyo niko vizuri tu na Nandy na haipendezi kioo cha jamii kugombana hovyo,” alisema Lulu Diva akiiambia Rick Media. 


Kauli ya Lulu Diva inakuja siku kadhaa baada ya Gigy Money kumshambulia Nandy kwa madai kuwa alichukua baadhi ya dili za kibiashara ambazo alistahili kuzipata.

OPEN IN BROWSER

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger