8/16/2020

Lyon yaiduwaza Man City na Kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa


Moussa Dembele aliingia uwanjani akitokea kwenye benchi la wachezaji wa akiba na kufunga mabao mawili ya dakika za mwisho wakati Lyon ikisababisha mshangao mwingine wa Ligi ya Mabingwa jana usiku, kwa kuiondoa Manchester City ya Pep Guardiola na ushindi wa mabao matatu kwa moja wa robo fainali mjini Lisbon.
City ilionekana kuwa kwenye mkondo sahihi wa kushinda mechi hiyo baada ya bao la Kevin De Bruyne katikati ya kipindi cha pili kulifuta bao la ufunguzi la Maxwel Cornet katika kipindi cha kwanza.

Lakini mambo yakaharibika wakati Dembele alipotumia makosa ya wachezaji wa City na kuipa Lyon ushindi. Lyon sasa itacheza nusu fainali Jumatano dhidi ya Bayern Munich.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger