8/23/2020

Maambukizi ya Corona yafikia watu Mil. 3 IndiaMaambukizi ya virusi vya corona nchini India yamefikia watu milioni 3 leo Jumapili na kulifanya taifa hilo kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi mapya huku ugonjwa huo ukidaiwa kuendelea kusambaa katika maeneo ya vijijini upande wa Kaskazini na Kusini mwa taifa hilo.


A health worker arrives at a mobile Covid-19 testing van in New Delhi, Aug. 16.


 


Maafisa wa afya wameripoti maambukizi mapya elfu 69,239 na vifo 912 nchini humo. Maambukizi zaidi yanasemekana kutokea katika miji mikubwa ya New Delhi na Mumbai.


Kwengineko nchini Ujerumani taasisi ya Robert Koch (RKI) ya magonjwa ya kuambukiza imesema idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona imeongezeka na kufikia 2,034 kwa siku na kufikisha idadi jumla ya watu 232,082, walioambukizwa.


Hadi kufikia sasa idadi ya watu milioni 23 wameambikzwa virusi hivyo duniani huku watu zaidi ya laki nane wakipoteza maisha.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger