8/19/2020

Madam Rita Kwa Mara ya Kwanza Afunguka Walivyomkataa Harmonize BSS "Harmonize alikuwa hajajiandaa"


Kama umeitazama video ya wimbo wa Jeshi ya msanii Harmonize kuna clip fupi inamuonyesha jinsi alivyopita kwenye mashindano ya BSS na kusema anawashukuru Master J na Rita kwa kumuongezea bidii baada ya kumkataa.


EATV & EA Radio Digital imepiga stori na Boss wa mashindano hayo ya BSS Madam Rita na amenyoosha maelezo jinsi ilivyotokea kwa kipindi kile hadi kufikia hatua ya kutompitisha kwenye mashindano hayo.

"Hatuna tatizo naye, ni msanii mzuri ila kipindi kile alivyopita alikuwa hajajiandaa sio kwamba tulimchukulia poa na tulikuwa hatumjui wala hatukumfanyia makusudi ila ni mambo ya kawaida na tunamkubali, tunafurahia anavyong'aa kwa sababu alipita pale, sekunde 30 huwezi ukaona kipaji cha mtu ila baada ya muda unaweza ukaona" ameeleza Madam Rita
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger