8/07/2020

Madhara ya Kujichubua kwa Watumiaji


Watu wengi hususani wanawake hupenda kuonekana wakiwa warembo, huku miongoni mwao wakiwa na dhana potofu ya kwamba ili uwe mrembo ni lazima ung'arishe rangi ya ngozi yako(Ujichubue).wapo wale wenye usemi ya baadhi ya wanaume kupenda wanawake weupe tamaa ambazo hupelekea-


Shinikizo la wanawake hao kutafuta vipodozi vya kupunguza weusi.

VIPODOZI VINAVYOTUMIKA KUJICHUBUA...

Vipodozi hivi huja katika aina tofauti,Wapo wanaotumia mafuta au dawa ya kung'arisha ngozi zao (lotion) au kumeza tembe. Au kama linavyojulikana kwa jina la Mkorogo. Suala hili linanipa motisha ya kulizamia kwa kina kujua athari za matumizi ya madawa ya kubadilisha ngozi ama kujichubua. (skin bleaching)

 KEMIKALI SUMU NDANI VIPODOZI...

Katika bidhaa zinazotumika kujichubua, kuna kemikali za aina mbili. Ambayo ni ‘Hydroquinone’ na ‘Mercury’
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira. pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele. Mercury nayo ni kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika maduka ya madawa.

 MADHARA YA KUJICHUBUA...

Katika kujichubua yapo madhara mbalimbali yanayowakumba watumiaji wa vipodozi hivyo;

Dkt. Elizabeth Kilili, ni mtaalamu na Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Product Limited ambaye ameainisha madhara yatokanayo na matumizi ya vipodozi hivyo ambayo ni pamoja na kupata kansa ya ngozi, kuzeeka mapema,kupata watoto wenye kasoro, mishipa ya fahamu,figo, kupungua kwa uzito na kupelekea athari za kuvunjika mifupa.Madhara haya huoneka mara moja na kadri mtu anavyozidi kutumia mkorogo kung'arisha ngozi yake.

Pia Dkt Kilili amesema, _“__upande wa mama mjamzito vipodozi venye viambata sumu vina muathiri mtoto kwenye mfumo wake wa chakula kupitia kitovu cha mama, kwa sumu inavyopita huelekea kwenye damu ambayo mtoto anapokuwa anazaliwa hutoka na kasoro tofauti ambazo huleta madhara katika ukuaji wake.”_

USHAURI WA KUZINGATIA...

Dkt Kilili anaendelea kwa kutoa ushauri wa kuepukana na madhara ya kujichubua huku akishauri matumizi ya bidhaa za asili zisizokuwa na madhara, ikiwemo kutumia vipodozi vilivyopitishwa na Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA) pamoja na kupata ushauri kwa wataalamu juu ya afya na magonjwa ya vipodozi ikiwemo kujikinga na madhara yanayoweza kupelekea athari katika mwili wako.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger