8/17/2020

Makosa yaliyoigharimu Man United dhidi ya SevillaKlabu ya Manchester United ilijikuta ikitupwa nje ya michuano ya Europa baada ya kipigo cha bao 2-1 walichokipata kutoka kwa Sevilla ya Hispania.


Ingawa Man United ilitangulia kupata bao la uongozi dakika ya tisa kwa mkwaju wa penati uliofungwa na Bruno Fernandes , hii ilipatikana kufuatia mshambuliaji Marcus Rashford kuchezewa madhambi kwenye eneo la hatari na Diego Carlos wa Sevilla.

Sevilla walisawazisha kupitia nyota wa zamani wa Liverpool, Suso aliyepachika bao kabla ya mapumziko lakini kipindi cha pili Luke De Jong alifunga bao la pili na la ushindi kwa Sevilla kunako dakika ya 78 na kuwapeleka fainali ambayo watacheza na mshindi kati ya Shaktar Donetsk na Inter Milan zitakazoumana usiku wa leo.

KIPI KILIIPONZA UNITED DHIDI YA SEVILLA?

1-Kumkosa mchezaji mwenye uwezo wa kumaliza mchezo,mfano mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, mshambuliaji wake Anthony Martial alipata nafasi ya wazi ambayo endapo angeitumia vyema, bila shaka angeiweka United kwenye nafasi nzuri ya kuongoza mchezo na kuongeza kujiamini kuliko ilivyokua.

Kazi nzuri ya kipa wa Sevilla, Yassine Bounou pia ilikua kikwazo kikubwa kwa Man United, lakini kukosekana kwa umakini kwa safu ya ushambuliaji, kuliigharimu sana Man United.

2-Makosa mawili kwenye safu ya ulinzi, mfano krosi iliyozaa bao la kwanza,Beki ya Kulia Aaron Wan Bissaka aliruhusu mpira kupita upande wake lakini pia si Victor Lindelof wala Harry Maguire aliyeuzuia mpira huo ambao ulipita moja kwa moja na kumkuta Suso aliyepachika bao maridadi kabisa.

JE MAN UNITED IMEFELI?

-Huu ni msimu mbaya kwa Man United , kwani wameondolewa kwa mara ya tatu kwenye nusu fainali, zikiwemo za Carabao Cup, FA Cup na sasa ya Europa League.

-Man United imekosa nafasi ya kutwaa taji la kwanza baada ya miaka mitatu tangu kuondoka kwa Jose Mourinho.

KIPI KIFANYIKE?

Wanapaswa kuhakikisha wanafanya usajili wa Jadon Sancho ambaye ana makali ya kucheka na nyavu ili kuimarisha safu ya ushambuliaji.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger